BEIRUT: Lebanon yaendelea kushambuliwa na Israel
16 Julai 2006Matangazo
Mashambulio ya Israel yameendelea kusini mwa Lebanon na kwenye vitongoji vilivyo kusini ya mji mkuu Beirut,ambavyo ni ngome za wanamgambo wa Hezbollah.Miongoni mwa vituo vilivyolengwa ni stesheni ya televisheni ya Hezbollah.Ndege za kivita za Israel zimeshambulia vituo vya kiraia vile vile,ikiwa ni pamoja na madaraja na barabara.Mashambulio hayo ya Israel yaliyoanza baada ya wanajeshi wake 8 kuuawa na wengine 2 kutekwa nyara na wanamgambo wa Hezbollah,yameua zaidi ya watu 100.