1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Lebanon imeomba rasmi msaada wa Ujerumani

7 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDEh

Serikali ya Lebanon imetoa ombi rasmi kwa Umoja wa Mataifa kuidhinisha kupelekwa kwa manowari za Ujerumani kupiga doria mwambao wake kwenye bahari ya Mediterania.Msemaji wa serikali ya Lebanon aliwaambia waandishi wa habari mjini Beirut kuwa ombi hilo limepelekwa katika barua iliyotumwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan.Hatua hiyo imechukuliwa muda mfupi baada ya serikali ya Israel kutangaza kuwa siku ya Alkhamisi, itaondosha vikwazo vya angani na baharini vilivyowekwa dhidi ya Lebanon.Israel iliweka vikwazo hivyo,ilipoanza kuwashambulia wanamgambo wa Hezbollah kati kati ya mwezi Julai.Iliendelea na vikwazo hivyo licha ya kupatikana makubaliano ya kusitisha mapigano hapo Agosti 14 chini ya upatanishi wa Umoja wa Mataifa.Azma ni kuzuia usafirishaji wa silaha kwa wanamgambo wa Hezbollah.Manowari za kijeshi za Ufaransa,Italia na Ugiriki zinatazamiwa kuwepo huko mpaka Ujerumani itakapopokea dhamana hiyo baada ya kama majuma mawili.