BEIRUT Kundi la Hizbolah latangaza ushindi katika uchaguzi wa Lebanon
6 Juni 2005Matangazo
Kundi la Hizbolah pamoja na kundi la Amal, ambayo ni washiriki wakubwa wa serikali ya Syria, yamejitangaza kuwa washindi wa uchaguzi mkuu wa Lebanon. Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa baadaye leo, lakini orodha ya makundi hayo mawili yalitangaza ushindi baada ya kushinda viti vyote 23 katika maeneo mawili ya uwakilishi bungeni kusini mwa nchi hiyo.
Uchaguzi huo mkuu, ambao ni wa kwanza kufanyika nchini Lebanon, tangu kuondoka kwa wanajeshi wa Syria, utaendelea kufanyika katika kila eneo kila mwishoni mwa juma hadi kufikia tarehe 19 mwezi huu.