1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT. Kiongozi wa usalama nchini Lebanon ajiuzulu.

25 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFJP

Kiongozi wa usalama mwenye usemi mkubwa nchini Lebanon, na anayeegemea upande wa Syria, Jamil al-Sayyed, amewasilisha barua ya kutaka kujiuzulu kutoka kwa wadhifa wake, muda mfupi kabla ya vikosi vya mwisho vya anajeshi wa Syria kuondoka nchini humo.

Hii ni kufuatia masharti yaliyotolewa na upinzani nchini humo ukiwataka wakuu wote watano wa usalama wajiuzulu baada ya mauaji ya waziri mkuu wa zamani, Rafik Hariri. Sayyed,a ambaye amekuwa ngome ya usalama nchini Lebanon kwa miaka saba, amesema amejiuzulu kwa sababu ya mabadiliko muhimu katika sera za maongozi zilizomutaeua madarakani.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Israel, Silvan Shalom, amesema Israel ina matumaini kwamba kuondoka kwa wanajeshi wa Syria kutoka Lebanon kutaifungulia milango amani mjini Beirut.