BEIRUT: Kambi ya wakimbizi yashambuliwa na vikosi vya Lebanon
23 Juni 2007Matangazo
Vikosi vya Lebanon vimeshambulia kambi ya wakimbizi wa Kipalestina,ya Nahr al-Bared, kaskazini mwa Lebanon.Mashambulio hayo yamefanywa baada ya wapiganaji wa kundi la Fatah al-Islam kumpiga risasi na kumuua mwanajeshi mmoja na kuwajeruhi 3 wengine kwenye kambi hiyo. Wanamgambo hao wamejificha huko baada ya kukimbia kutoka maeneo ya jirani yaliyodhibitiwa na vikosi vya serikali.Maafisa wa majeshi ya Lebanon wamesema,hawatositisha mashambulio yake dhidi ya kambi hiyo,mpaka wanamgambo wote watakaposalim amri.