1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Jeshi la Lebanon laongeza mashambulio dhidi ya wanamgambo

25 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBfL

Jeshi la Lebanon limeongeza mashambulio dhidi ya kambi ya wakimbizi wa kipalestina ya Nahr el Bared kaskazini mwa Lebanon.

Lengo la harakati hiyo ni kuliteka eneo la mwisho ambalo mpaka sasa bado linadhibitiwa na wanamgambo wa kundi la Fatah al Islam.

Mashambulio hayo ya maroketi yanafuatia mapambano makali wakati ambapo wanajeshi walifaulu kuingia maeneo yaliyo ndani ya kambi ya Nahr el Bared kuwachakaza wanamgambo waliosalia katika kambi hiyo.

Mapigano baina ya wanajeshi wa Lebanon na wanamgambo wa kundi la Fatah al Islam yalianza mnamo tarehe 20 mwezi Mei mwaka huu na kufikia sasa watu zaidi ya 200 wameuwawa wakiwemo wanajeshi 118.

Karibu wakaazi wote 31,000 wa kambi ya Nahr el Bared wamehamishwa, lakini inaripotiwa wake 20 na watoto 45 wa wapiganaji wamo ndani ya kambi hiyo licha ya kutakiwa waondoke na jeshi la Lebanon.