1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Jeshi la Lebanon lajiandaa kuivamia kambi ya wakimbizi ya Nahr al Bared

11 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBjj

Jeshi la Lebanon linajiandaa kuwavamia wanamgambo wa kiislamu walio katika kambi ya wakimbizi ya Nahr el Bared kaskazini mwa Lebanon.

Wanajeshi wa Lebanon wamekuwa wakipambana na wapiganaji wa kundi la Fath al Islam lenye mafungamano na kundi la al- Qaeda ndani ya kambi ya Nahr al Bared kwa wiki nne.

Mwezi uliopita, jeshi la Lebanon liliziteka ngome za wanamgambo wa kundi hilo nje ya kambi hiyo. Wanajeshi takriban 87, wanamgambo 75 na raia 43 wameuwawa tangu mapigano yalipozuka mnamo tarehe 20 mwezi Mei mwaka huu.

Mkataba uliosainiwa na nchi za kiarabu mnamo mwaka wa 1969 uliwapiga marufu wanajeshi wa Lebanon kuingia kambi za Wapalestina, lakini mkataba huo ukafutiliwa mbali na bunge la Lebanon katikati ya miaka ya 1980, ingawa umekuwa ukitekelezwa.