1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT/JERUSALEM: mapigano kumalizwa nchini Lebanon

14 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDLs

Waziri Mkuu wa Israel bwana Ehud Olmert ameyaamrisha majeshi ya nchi yake kuanza kutekeleza azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa juu ya kumaliza mapigano nchini Lebanon.

Baadhi ya majeshi ya Israel yataondolewa kutoka kusini mwa Lebanon na mengine kiasi yatabakia , ili kukabidhi ulinzi kwa jeshi la kimataifa.

Lakini wakati huo huo idara za usalama za Lebanon zimesema watu 17 waliuawa katika mashambulio yaliyofanywa na ndege za Israel nchini kote.

Ndege hizo zilifanya mashambulio makubwa hasa katika vitongoji vya kusini mwa mji wa Beirut.

Na habari zaidi zinasema kwamba wapiganaji wa Hezbollah pia walifanya mashambulio ya roketi katika kiwango ambacho hakikuwahi kufanyika mnamo kipindi cha siku moja tokea kuanza mgogoro wa Lebanon wiki nne zilizopita.

Jeshi la Israel limetaarifu kwamba askari wake watano wameuawa na wengine 25 wamejeruhiwa.