BEIRUT: Israel yaendelea kuishambulia Lebanon
14 Julai 2006Uwanja wa ndege wa Beirut nchini Lebanon kwa mara ya tatu katika muda wa saa 24,umeshambuliwa kwa mabomu na vikosi vya angani vya Israel.Hapo awali,mashambulio ya ndege za kijeshi za Israel yalilenga vitongoji vilivyo kusini mwa mji mkuu Beirut,vilivyodhaniwa kuwa ni ngome za wanamgambo wa Hezbollah.Mashambulizi ya Israel yamelenga pia kinu cha umeme,barabara ya kwenda uwanja wa ndege wa Beirut na hata barabara kuu ya Beirut kuelekea mji mkuu wa Syria,Damascus.Wakati huo huo Israel imefunga bandari zote nchini Lebanon.Ripoti zasema zaidi ya watu 50 wameuawa nchini Lebanon.Kwa upande mwingine,makombora ya Hezbollah yaliyoangukia kaskazini mwa Israel yameuwa raia 2 wa Kiisraeli.Mgogoro huu ulizuka baada ya wanajeshi 8 wa Kiisraeli kuuawa na wengine 2 kutekwa nyara na wapiganaji wa Hezbollah waliyokivamia kituo cha kijeshi mpakani.