1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Israel yaendelea kuishambulia Lebanon

18 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG6V

Mashambulio ya angani ya Israel yameua watu wengine 6 nchini Lebanon,huku serikali za kimataifa zikijaribu kuwahaamisha raia wake kwa njia ya meli.Sasa,idadi ya watu waliouawa katika mashambulio ya Israel muda wa siku sita za nyuma,imefikia 210.Wengi wao ni raia wa kawaida. Mashambulio ya hivi karibuni yalilenga kijiji cha Aitaroun mpakani mwa Lebanon na kambi ya maaskari wa Lebanon karibu na Beirut.Wanamgambo wa Hezbollah vile vile,kutoka kusini mwa Lebanon, walishambulia kwa makombora eneo la kaskazini la Israel.Makombora hayo tena yamefika hadi Haifa na Waisraeli 4 wamejeruhiwa.Kombora lililoangukia karibu na hospitali mjini Safe,liliwajeruhi watu 5.Juhudi za kuwahamisha raia wa kigeni kutoka Lebanon zikiendelea,meli zilizopelekwa na Ufaransa na Italia zimeshaondoka Beirut kuelekea Cyprus.Wakati huo huo,Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan ametoa mwito wa kupelekwa kikosi cha kimataifa kusini mwa Lebanon.