1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Israel yaendelea kuishambulia Lebanon

4 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDOy

Ndege za kivita za Israel kwa usiku wa pili kwa mfululizo zimeshambulia tena eneo lililo kusini mwa mji mkuu wa Lebanon,Beirut.Wakati huo huo waziri wa ulinzi wa Israel,Amir Peretz ameliamuru jeshi kujitayarisha kusonga mbele kaskazini mwa mpaka wa Israel na kwenda hadi mto Litani ulio kama kilomita 20 ndani ya ardhi ya Lebanon.Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya ulinzi ya Israel,lengo ni kulidhibiti eneo la kusini la Lebanon na kuwangóa wanamgambo wa Hezbollah kutoka eneo hilo.