1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT. Duru ya tatu ya uchaguzi nchini Lebanon

12 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF4I

Wananchi wenye haki ya kupiga kura nchini Lebanon hii leo wanashiriki katika duru ya tatu kutoka jumla ya duru nne za uchaguzi.Wagombea kura wanapigania viti vya eneo la katikati la Mount Lebanon na mashariki mwa Bonde la Bekaa.Takriban nusu ya viti 128 vya bunge,vinagombewa katika maeneo hayo,kwa hivyo hii ni duru muhimu ya uchaguzi.Huu ni uchaguzi wa mwanzo kupata kufanywa tangu Syria kuondosha vikosi vyake kutoka Lebanon baada ya kuwepo nchini humo kwa kipindi cha miaka 30.Vyama vinavyoipinga Syria vinatazamiwa kushinda viti vingi bungeni,vikiungwa mkono na wengi waliohuzunishwa na mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa Lebanon,Rafik al-Hariri.Mwanasiasa huyo aliuawa katika mripuko wa bomu mwezi wa Februari.Kwa upande mwingine,Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan siku chache za nyuma aliamua kuipeleka tena Lebanon tume ya kuchunguza madai kwamba maajenti wa upelelezi wa Kisyria,bado wapo nchini Lebanon.