1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut. Blair aahidi kuijenga upya Lebanon.

12 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDDE

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair ameahidi kutoa msaada wa kuijenga upya Lebanon iliyoharibiwa na vita, wakati wa ziara yake ya kwanza mjini Beirut mapema jana Jumatatu.

Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kufuatia mazungumzo na waziri mkuu Fuad Siniora.

Blair na Siniora wamesema kuwa utatuzi wa mgogoro wa Israel na Palestina ni muhimu kuweza kuleta hali imara katika eneo hilo.

Mkutano huo na waandishi wa habari uliingiliwa kati na mwanamke mmoja aliyekuwa akipinga msimamo wa Blair katika mzozo wa Israel na Hizbollah.

Nje ya ukumbi huo wa mkutano , kiasi cha watu 2,000 walikuwa wakiandamana wakipinga ziara ya Blair, wakimshutumu kwa kuunga mkono vita vya siku 34 vya Israel na wapiganaji wa Hizbollah na mawaziri kadha wa Hizbollah wamekataa kukutana nae.