1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Bakri akamatwa la polisi nchini Lebanon

11 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CElq

Polisi nchini Lebanon imemkamata muislamu mwenye itikadi kali, Omar Bakri, anayechunguzwa na Uingereza kwa matamshi yake juu ya mashambulio ya mabomu ya Julai saba mjini London. Lakini polisi ya Uingereza imesema hakuna waranti iliyotolewa ya kukamatwa kwake.

Serikali ya Uingereza inawazuilia raia kumi wa kigeni wanaotuhumiwa kuwa hatari kwa usalama wa taifa. Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani nchini humo amekataa kuyataja majina ya washukiwa hao lakini akasema watarudishwa nchini kwao.

Juma lililopita waziri mkuu wa Uingereza bwana Tony Blair alitangaza sheria kali zinazolenga kuirihusu serikali yake kuwarudisha nchini kwao waislamu wenye itikadi kali.