1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING:Wanaharakati wa Tibet wafukuzwa China

9 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBam

China imewarudisha makwao kundi la wanaharakati wa Tibet ambao walibandika bango kwenye ukuta mashuhuri nchini humo wakidai uhuru wa jimbo la Tibet.Wanaharakati hao wanane wako Hongkong baada ya kukaa korokoroni kwa siku mbili huko China.

Hapo jana China ilifanya sherehe kabambe katika uwanja wa Tianamen Square kuadhimisha kutimia mwaka mmoja kabla ya kufungua mashindano ya mwaka 2008 Olimpiki.

China imekuwa ikikosolewa katika siku za hivi karibuni na wapinzani wake pamoja na wakosoaji kutoka nje ambao wanasema nchi hiyo inadhihaki umuhimu wa utu katika Olimpiki kwa kuzidi kukiuka haki za binadamu.