BEIJING:mkutano wa G20
15 Oktoba 2005Matangazo
Rais Hu Jintao wa China ametaka kuwepo kwa maendeleo juu ya kuondosha vikwazo vya kibiashara duniani na kupambana na umaskini.
Katika mkutano wa siku mbili wa kile kinachoitwa mataifa ya G20 masuala mengine yatakayojadiliwa ni athari ya ongezeko la bei ya mafuta ambayo huenda ikaathiri uchumi duniani na mipango ya mageuzi ya shirika la fedha duniani IMF na Benki ya Dunia.
G20 inajumuisha mataifa saba yanayoongozwa kiviwanda duniani na mataifa yote makubwa yanayoendelea.