1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING:Dhoruba yasababisha hasara ya maisha na mali

18 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG6c

Vyombo vya habari nchini China vinasema kuwa hadi watu 170 wameuawa katika mafuriko ya maji na matope yaliyosababishwa na dhoruba iliyopewa jina “Bilis”.Zaidi ya watu mia kadhaa pia hawajulikani walipo,baada ya dhoruba hiyo kuvuma katika eneo la kusini-mashariki,mwishoni mwa juma lililopita. Katika wilaya ya Hunan,makundi ya wasaidizi na wanajeshi yalipelekwa katika eneo hilo kusaidia kuwaokoa watu waliyonasa katika mafuriko.Kwenye wilaya ya Fujia ambako dhoruba na mvua zilisababisha mmomonyoko wa ardhi,takriban nyumba 20 elfu zimesombwa na matope.Zaidi ya watu nusu milioni wamehamishwa kutoka maeneo yaliyoathirika.