BEIJING: Zimbabwe na Uchina kushirikiana kiuchumi
27 Julai 2005Matangazo
Vyombo vya habari nchini Uchina vimeripoti kuwa serikali ya Beijing na Zimbabwe zitashirikiana kiuchumi.Kampuni moja ya kiserikali nchini Uchina imetia saini mapatano ya mkopo,kukitanua kinu cha nishati cha Hwange nchini Zimbabwe.Vile vile Zimbabwe itauziwa ndege aina ya MA60.Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe alikwenda Beijing kujaribu kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi pamoja na Uchina.Madola mengi ya magharibi yamejiweka mbali na Mugabe,akituhumiwa kukiuka haki za binadam