BEIJING: Waziri mkuu wa Japan ziarani China
8 Oktoba 2006Matangazo
Waziri mkuu mpya wa Japan,Shinzo Abe amewasili China.Abe ni waziri mkuu wa kwanza wa Japan kuitembelea China tangu miaka mitano ya nyuma.Lengo la ziara yake ni kupunguza mivutano kati ya madola hayo mawili makuu,yenye uchumi mkubwa kabisa barani Asia.Siku ya Jumatatu,Abe ataelekea Korea ya Kusini huku wasi wasi ukizidi kuhusu Korea ya Kaskazini ambayo juma lililopita ilitishia kujaribu bomu lake la kwanza la kinuklia.Kwa maoni ya viongozi wa China na Japan,serikali ya Pyongyang inaweza kufanya jaribio hilo wakati wo wote ule.