1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: Msaada kwa Korea Kaskazini badala ya mradi wa nyuklia

8 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCTx

Korea ya Kaskazini imeashiria huenda ikakubali kuachilia mbali mradi wake wa kutengeneza silaha za kinyuklia.Mjumbe wa serikali ya Pyongyang,Kim-Kye-Gwan amesema,uwezekano huo upo lakini hilo hutegemea thibitisho la Marekani.Hatua hiyo imetokea wakati ambapo kundi la nchi sita linajadiliana mjini Beijing,katika duru mpya ya mazungumzo kuhusu mradi wa nyuklia wa Korea ya Kaskazini.Mjumbe wa Marekani katika majadiliano hayo,Christopher Hill,hapo awali alisema kuwa anaamini Korea ya Kaskazini inaweza kushawishiwa kutekeleza makubaliano ya mwaka 2005 kuachilia mbali mradi wake wa kinuklia na badala ya kupewa msaada,manufaa katika sekta ya nishati na kuhakikishiwa usalama wake.Duru hii mpya ya majadiliano kati ya China,Japan,Marekani,Urussi, Korea ya Kaskazini na Korea ya Kusini inafanywa miezi minne baada ya Korea ya Kaskazini kufanya jaribio lake la kwanza la nyuklia.