1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: Mazungumzo juu ya silaha za nyuklia yaanza tena

26 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEqc

Mazungumzo juu ya mpango wa nyuklia wa Korea ya kaskazini yanaendelea mjini Beijing China.

Mjumbe wa Korea bwana kim Kye Gwan amesema kwamba, nchi yake inadhamiria kuchukua hatua za kuondolewa kwa mvutano wa kijeshi baina ya Korea mbili ,ikiwa kama Marekani kwanza itaihakikishia usalama nchi yake.

Akizungumza kwenye mkutano huo, naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani bwana Christopher Hill amesisitiza umuhimu wa kuondoa silaha zote za nyuklia katika eneo lote la Korea.

Mapema mwaka huu Korea ya Kaskazini ilitangaza rasmi kuwa ina silaha za nyuklia.

Mkutano huo wa Beijingi unahudhuriwa pia na wajumbe kutoka Korea ya kusini,China,Urusi na Japan

Mazungumzo juu ya mpango wa nyuklia wa Korea ya Kaskazini yalivunjika mwaka mmoja na nusu uliopita baada ya Korea ya Kaskazini kukataa kurejea kwenye meza ya mazungumzo.

.