BEIJING: Majadiliano kuhusu mradi wa nyuklia wa Korea Kaskazini
8 Februari 2007Matangazo
Duru mpya ya mazungumzo ya kundi la pande sita yameanza mjini Beijing.Lengo la majadiliano hayo yanayohudhuriwa na China,Japan,Urussi,Marekani, Korea ya Kaskazini na Korea ya Kusini ni kuishawishi Korea ya Kaskazini kuachilia mbali mradi wake wa nyuklia.Oktoba mwaka jana,hali ya wasi wasi iliongezeka baada ya serikali ya Pyongyang kufanya jeribio lake la kwanza la nyuklia.Siku chache baadae,Umoja wa Mataifa ukachukua hatua ya kuiwekea vikwazo Korea ya Kaskazini.