1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: Mada kuu ni miradi ya nyuklia ya Iran na Korea ya Kaskazini

3 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCMs

Makamu wa waziri wa nje wa Marekani,John Negroponte,amewasili mji mkuu wa China,Beijing kukutana na viongozi wa nchi hiyo.Mada kuu ya majadiliano yao ni masuala yanayohusika na nchi hizo mbili na pia miradi ya nyuklia ya Iran na Korea ya Kaskazini.Hapo awali Negroponte alikuwepo Tokyo ambako alikutana na wajumbe wa serikali ya Japan kujadili matatizo hayo hayo.Kabla ya kuondoka Tokyo Negroponte alisema, Korea ya Kaskazini lazima ichukue hatua za kutosha kusitisha mradi wake wa silaha za nyuklia,kabla ya Marekani kuondosha vikwazo vya kiuchumi na kuitoa Korea ya Kaskazini kutoka orodha ya nchi zinazotuhumiwa kuunga mkono ugaidi.Lakini wizara ya fedha ya Marekani,siku ya Ijumaa,iliashiria kuwa vikwazo huenda vikaregezwa juma lijalo.