1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing: Kansela Gerhard Schröder wa Ujerumani amekosoa vikali mitindo...

3 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFvh
ya kuandamwa na kukamatwa "wana mtandao wa internet" kataika jamhuri ya umma wa China.Akiwahutubia wanafunzi katika mji wa bandari wa Kanton,kansela Gerhard Schröder amesema China italifikia lengo lake la kugeuka taifa lenye wana mtandao wengi kabisa ulimwenguni,itakaporuhusu na kurahisisha mawasiliano kwa njia ya internet katika daraja ya kitaifa na kimataifa.Kansela Schröder amesema uhuru wa waenezaji na watumiaji wa mtandao wa internet ndio msingi wa kulifikia lengo hilo.Wakati huo huo nchini Ujerumani kwenyewe kumezuka upinzani miongoni mwa wanachama wa chama shirika katika serikali ya muungano-Die Grüne,dhidi ya kuuziwa China mtambo wa kinuklea wa Hanaue."Walinzi wa mazingira wanahoji "haiwezekani kwanza kuamua kuufunga mtambo huo na baadae kuufanyia biashara nchi za nje.Kansela Gerhard Schröder ameahidi kuzingatia maombi ya China ya kuununua mtambo huo wa nguvu za kinuklea.