1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing. Japan na China zakwama katika mzozo wa kidiplomasia

18 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFLs

.

Mzozo wa kidiplomasia kati ya Japan na China umesababisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili kuwa katika hali mbaya tangu kuanzishwa mwaka 1972. Hali hiyo imejitokeza licha ya ziara ya waziri wa mambo ya kigeni wa Japan Nobutaka machimura kwa mazungumzo na waziri mwenzake wa China Li Zhaoxing. Baada ya wiki kadha za maandamano ya kuipinga Japan , Li amesema serikali yake haiwezi kuomba radhi, kwa sababu serikali ya Japan imefanya vitendo kadha ambavyo vimeathiri hisia za watu wa China. Maandamano hayo yalizuka kutokana na Japan kuidhinisha kitabu kipya cha historia kitakachotumika mashuleni ambacho waandamanaji wanasema kinapuuzia ukatili uliofanywa na Japan katika vita vikuu vya pili vya dunia. Waandamanaji pia wanapinga dhidib ya juhudi za Japan kutaka kuwa na kiti cha kudumu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa.