1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: Dhoruba yasababisha hasara ya maisha na mali

17 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG6x

Dhoruba ya majira ya joto iliyopewa jina “Bilis” imeua watu wasiopungua 115 na kujeruhi mamia wengine kusini-mashariki mwa China.Dhoruba hiyo ikivuma na ikingóa mapaa,serikali imelazimika kuwahamisha wafungwa kutoka jela moja na wakazi wa vijijini kwa maelfu.Dhoruba iliyoanza kuvuma tangu siku ya Ijumaa,imeteketeza nyumba na barabara na vile vile umeme umekatika.Kwenye wilaya ya Fujian,iliyoathirika vibaya zaidi kusini-mashariki mwa nchi,hadi watu 43 wamepoteza maisha yao.Wengine 39 wamefariki katika wilaya ya ndani ya Hunan na 33 katika wilaya ya Guangdong inayopakana na Hong Kong upande wa kusini.