1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing. Costa Rica yaitupa mkono Taiwan.

7 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBu6

Costa Rica imekatisha karibu miaka 60 ya uhusiano wake wa kibalozi na Taiwan na kuitambua China. Rais wa Costa Rica Oscar Arias amesema kuwa nchi yake ina haja ya kuvutia vitega uchumi kutoka China na haiwezi tena kupuuzia uzito wa uchumi wa China.

Mabadiliko hayo yanaiacha Taiwan , ambayo China inaitambua kama jimbo lake lililojitenga , kuwa imebaki na mahusiano ya kibalozi na nchi 24 nyingi zikiwa nchi ndogo ndogo, nusu yake zikiwa Latin America.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Taiwan James Huang ameishutumu Costa Rica kwa kuihadaa nchi hiyo katika muda wa wiki chache zilizopita kuhusiana na mabadiliko hayo.

Mwaka jana biashara kati ya Costa Rica na China iliongezeka mara dufu kwa kiasi cha dola milioni 500. Tangu mwaka 2001 China imeweza kuzivuta nchi nane washirika wakubwa wa Taiwan, ikiwa ni pamoja na Chad na Macedonia.