1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING. China yaitaka Japan kuipoza hasira ya wachina.

11 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFOQ

Japan ni lazima ichukue hatua zaidi kupoza hasira ya umma wa China na kuuendeleza uhusiano kati ya mataifa hayo mawili. Matamshi haya yametolewa na msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni wa China, Qin Gang, kufuatia maandamano ya siku mbili ya kuipinga Japan. Maandamano hayo yalifanywa na wachina waliokasirishwa na hatua ya Japan kujaribu kuyafunika mateso ya vita vya pili vya dunia na juhudi zake za kutafuta kiti cha kudumu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa. Wakati huo huo, tetemeko la ardhi limetokea mashariki mwa Tokyo, mapema leo. Tetemeko hilo lililokuwa la kipimo cha Richter 6.1, halikusababisha uharibifu mkubwa. Huduma za magarimoshi yanayosafiri kwa kasi na usafiri wa ndege katika kiwanja cha Narita ulitatizwa kwa muda mfupi.