Beijing. China ya ongeza thamani ya sarafu yake.
22 Julai 2005China imeacha kuiweka sarafu yake katika mlingano na dola ya Marekani, kufuatia miezi kadha ya mbinyo kutoka Marekani kuweza kuiacha sarafu hiyo ijitafutie thamani kutokana na nguvu ya masoko.
Sarafu ya China ilithaminiwa upya na kupanda kwa zaidi ya asilimia 2, ikiwa ni ongezeko la kwanza katika muda wa kiasi miaka kumi.
China imesema kuwa thamani ya sarafu yake ya Yuan itafungamanishwa na jumla ya safaru nyingine kadha za mataifa mbali mbali ambayo hayakutajwa hapo baadaye.
Marekani imekuwa ikilalamika kuwa thamani ya Yuan isiyobadilika ilikuwa ni chini ya kiwango chake halisi, na hali hiyo ilikuwa inazipa bidhaa za China unafuu kinyume na haki.
Ujerumani, Uingereza na Japan zimeikaribisha hatua hiyo, zikisema kuwa hatua hiyo itakuwa nzuri kwa ajili ya ukuaji wa uchumi wa China.