1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Usalama wa chakulaKimataifa

Bei ya mchele yaongezeka zaidi Ulimwenguni

8 Septemba 2023

Bei ya mchele duniani iliongezeka mwezi Agosti kwa kiwango cha juu zaidi kuwahi kushuhudiwa katika miaka 15 iliyopita.

https://p.dw.com/p/4W6ll
Afrika Ghana Accra Markt
Picha: OLIVIER ASSELIN/AP/picture alliance

Inakadiriwa kuwa bei ya mchele duniani ilipanda kwa silimia 9.8 ikilinganishwa na mwezi uliotangulia.

Kulingana na shirika la Chakula na Kilimo duniani FAO, hali hiyo ilijiri baada ya msafirishaji mkuu wa nafaka hiyo India kupiga marufuku baadhi ya mauzo ya nje.

Mchele ni chakula kikuu duniani na bei yake katika  masoko kimataifa  imekuwa ikipanda kutokana na janga la Covid, vita vya Ukraine na athari za hali ya hewa mfano Elnino kwenye uzalishaji.

Shirika la FAo limesema, kutokuwa na uhakika juu ya muda wa marufuku hiyo na vikwazo vya mauzo ya nje vilisababisha wadau kwenye mnyororo wa uzalishaji kuhodhi bidhaa hiyo, ili kujadili upya mikataba au kuacha kutoa ofa za bei.