1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern yabaki na mechi moja tu kubeba ubingwa

15 Juni 2020

Muendelezo wa Bayern Munich wa matokeo mazuri umewakumbusha wapinzani wao ni nani jogoo anayewika katika Bundesliga na ushindi mwingine dhidi ya Werder Bremen kesho Jumanne utawahakikishia taji lao la nane mfululizo.

https://p.dw.com/p/3dnmZ
Fußball Bundesliga FC Bayern - Mönchengladbach
Picha: Getty Images/A. Hassenstein

Kutawala kwa klabu hiyo kumekuwa kumekuwa kitu cha kawaida tangu Borussia Dortmund iliposhinda ubingwa wa ligi 2012 kwa mara ya mwisho.

Bayern wameshinda mechi 13 mfululizo katika mashindano yote yamewaweka Bayern kilele na pengo la pointi saba huku ikiwa imesalia mechi tatu tu msimu kukamilika. Bayern walipata ushindi wa 2 – 1 dhidi ya Borussia Moenchengladbach Jumamosi na mmoja wa wachezaji ambao wanaibeba timu hiyo kwa sasa Leon Goretzka anasema macho yao yameangazia tu kwa taji "Nadhani leo ulikuwa ni mchezo mgumu sana lakini wenye matokeo mazuri kwetu. Ulikuwa wa nguvu na tukalazimika kukimbia sana, lakini nadhani sote tulionyesha uwanjani nia ya kushinda katika hatua ya mwisho na na mwishowe nadhani ushindi huo ulikuwa sawa".

Nambari mbili Borussia Dortmund watawaalika Mainz Jumatano, wakifahamu wazi kuwa wao wanawinda tiketi ya Champions League na sio taji la ligi. Dortmund walipata ushindi wa 1 – 0 dhidi ya Fortuna Duesseldorf mwishoni mwa wiki katika mechi ambayo mlinda mlango wa BVB Roman Burki alikiri kuwa ilikuwa ngumu "Tulikuwa na matatizo mengi ya kucheza kandanda letu uwanjani. Mara nyingi tulicheza kwa kujikokota sana na haikuwa siku nzuri kwa hivyo ushindi huu ulikuwa wa kibahati.

RB Leipzig watapiga dhidi ya Duesseldorf katika mechi ambayo wanahitaji ushindi ili kukamata nafasi ya champions League kama Gladbach watapoteza nyumbani dhidi ya Wolfsburg wakati timu ya nambari tano itakutana na ya nambari sita kesho.

Gladbach ipo kwenye king'anyiro na nambari nne Leverkusen cha tiketi ya mwisho ya Champions League. Leverkusen watawaalika watani wao wa mjini Cologne Jumatano baada ya kutoka sare bya 1 – 1 na Schalke jana Jumapili.