Bayern waweka rekodi mpya
6 Oktoba 2022Katika mechi 31 za makundi mabingwa hao wa Ujerumani hawajapoteza hata moja wakiipiku rekodi iliyowekwa na Real Madrid.
Wamefunga mabao tisa katika mechi zao mbili za mwisho katika michuano yote baada ya ushindi wa 4-0 wa ligi dhidi ya Bayer Leverkusen Jumamosi na kuhitimisha msururu wa michezo minne bila kushinda katika Bundesliga.
Leroy Sane alitikisa wavu dakika ya saba, Serge Gnabry akaongeza la pili dakika tano baadaye na Sadio Mane dakika ya 21 yaliwaweka katika nafasi nzuri kimchezo.
Der Klassiker
Bavarians, ambao watamenyana na Borussia Dortmund katika Der Klassiker ya Bundesliga siku ya Jumamosi, hawakupata upinzani wowote kutoka kwa timu hiyo kutoka jamuhuri ya Czech na walitumia vyema mapungufu makubwa katika safu yao ya ulinzi katika kila fursa.
Licha ya kukosekana kwa Thomas Mueller na Joshua Kimmich kwa sababu ya COVID-19, waliwashinda wapinzani wao kupanga mchezo na kupigiana pasi nzuri, na Jamal Musiala alipaswa kufanya matokeo kuwa 4-0 katika dakika ya 25 wakati alikuwa na kipa pekee lakini akaipoteza nafasi.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani alifanya marekebisho katika dakika ya 36 alipopiga kombora lililompita mlinda lango Marian Tvrdon, lakini juhudi zake zilikataliwa kuwa ameotea.
Bayern, hata hivyo, waliendelea pale walipoishia baada ya kipindi cha mapumziko Sane akiifungia pasi ya Mane iliyoinuliwa kwa kasi dakika tano baada ya mchezo kuanza tena.
Mchezaji wa akiba Eric Maxim Choupo-Moting alifunga kwa shuti kali nje ya lango na kukamilisha kinyang'anyiro hicho na kuwaweka Bayern kileleni mwa kundi kwa pointi tisa kutokana na michezo mitatu waliyocheza.
Inter Milan na Barcelona, zote zikiwa na pointi tatu, zitamenyana siku ya Jumanne.
//Reuters