1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern wana kibarua ugenini London

19 Februari 2013

Kushindwa kwa Bayern Munich kunyanyua taji kuu la kandanda barani Ulaya tangu mwaka wa 2001, licha ya kufika kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa mara mbili katika misimu mitatu iliyopita, kunawapa motisha miamba hao

https://p.dw.com/p/17gwZ
Munich's Croatian forward Mario Mandzukic (2nd L) is congratulated by his teammates Munich's Spanish midfielder Javier Martinez (L), Munich?s midfielder Bastian Schweinsteiger (2nd R) and Munich?s Austrian defender David Alaba (R) after scoring the 0-1 during the German first division Bundesliga football match between VfB Stuttgart and Bayern Munich in Stuttgart, southwestern Germany, on January 27, 2013. AFP PHOTO / THOMAS KIENZLE RESTRICTIONS / EMBARGO - DFL RULES TO LIMIT THE ONLINE USAGE DURING MATCH TIME TO 15 PICTURES PER MATCH. IMAGE SEQUENCES TO SIMULATE VIDEO IS NOT ALLOWED AT ANY TIME. FOR FURTHER QUERIES PLEASE CONTACT THE DFL DIRECTLY AT + 49 69 650050. (Photo credit should read THOMAS KIENZLE/AFP/Getty Images)
Fußball 1. Bundesliga 19. Spieltag Vfb Stuttgart FC Bayern MünchenPicha: Getty Images

Bayern ambao walishindwa mnamo tarehe 28 Oktoba, hawajafungwa goli katika mwaka huu wa 2013 na wana uongozi wa tofauti ya pointi 15 kileleni ligi ya nyumbani Bundesliga. Na sasa leo wanacheza ugenini dhidi ya Arsenal katika mechi y amkondo wa kwanza wa awamu ya mchujo katika Champions League. Mkufunzi wa Bayern Jupp Heynckes anafahamu kwamba ni lazima anyakue taji hilo msimu huu kabla ya kumwachia usukani mwezi Julai aliyekuwa mkufunzi wa Barcelona Pep Guardiola.

Heynckes, mwenye umri wa miaka 67, na mchezaji wa zamani wa Ujerumani ambaye alishinda kombe la Champions League kama kocha wa Real Madrid mwaka wa 1998 amekuwa na mwanzo mzuri katika msimu wake wa pili na Bayern baada ya kuambulia patupu katika msimu wa 2012.

Anasema kikosi chake kimeimarika na hasa katika safu ya ulinzi, na ni muhimu kwa wachezaji kulinda lango lao vyema na vile vile kushambulia kwa kasi. Heynckes anasema wana ari kubwa ya kushinda mataji na hilo litabainika wakati vijana wake watakapojitosa katika uwanja wa Emirates leo usiku kumenyana na Arsenal.

Akizungumza kabla ya mchuano wa leo, mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger alionekana mwenye mchanganyiko wa hisia katika kikao cha waandishi wa habari. Wenger alikabiliwa na shutuma kali kutoka kwa mashabiki na wachambuzi wa soka baada ya kubanduliwa nje ya kombe la FA kwa kufungwa goli moja wka sifuri na Blackburn Rovers. Mfaransa huyo anasema kitu cha maana siyo kile watu wanasema, bali kile wanachoonyesha katika uwanja wa kabumbu.

Lukas Podolski atacheza dhidi ya klabu yake ya zamani
Lukas Podolski atacheza dhidi ya klabu yake ya zamaniPicha: AP

Anasema ni lazima vijana wake waonyeshe bidii na nguvu kiakili ili kukabiliana na maoni yoyote. Kocha huyo anasumbuliwa kichwa na safu ya ulinzi kwa sababu Laurent Koscielny hayuko katika hali shwari. Lukas Podolski huenda akaanzishwa kikosini dhidi ya klabu yake ya zamani.

Katika mpambano mwingine wa leo, FC Porto na Malaga zitatoana kijasho nchini Ureno. Porto hawajashindwa katika mechi 19 za mwisho katika ligi ya nyumbani na wanaongoza ligi kwa pamoja na Benfica na tofauti ya pointi 14.

Malaga nayo iko katika nafasi ya nne katika La liga ya Uhispania na wamecheza mechi tano bila kushindwa. Mkufunzi wa Porto Vitor Perreira anasema mchuano huo utakuwa moto wa kuotea mbali. Mshambuliaji wake Mcolombia Jackson Martinez ndiye tegemeo. Katika safu ya kiungo kuna Muargentina Lucho Gonzalez na Mreno Joao Moutinho. Mghana Christian Atsu pia amerudi kikosini kutoka katika fainali za kombe la mataifa ya Afrika AFCON. Wachezaji wa pembeni James Rodriguez na Silvestre Varela wamerejea kikosini. Kesho Jumatano AC Milan watakabana koo na Barcelona, wakati Galatasaray wa Uturuki wakiangushana na Schalke 04 wa hapa Ujerumani.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters

Mhariri: Daniel Gakuba