1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern munich ziarani Japan

Ramadhan Ali31 Julai 2006

Wakati mabingwa wa Ujerumani wanajinoa leo huko Japan kwa Bundesliga, Enyimba ya Nigeria yashindwa kutamba mbele ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini.Katika riadha, justin Gatlin bingwa wa olimpik na dunia mita 100 achunguzwa kwa madham bi ya doping.Michael Schumacher atamba katika mbio za magari za Hockenheim,Ujerumani:

https://p.dw.com/p/CHdS
Michael Schumacher atamba nyumbani Hockenheim.
Michael Schumacher atamba nyumbani Hockenheim.Picha: AP

Mabingwa wa Ujerumani-Bayern Munich wanacheza leo nchini Japan na Urawa Reds.

Bayern Munich ikijinoa kwa msimu mpya wa Bundesliga,iliwasili jana Japan kwa mpambano wa kirafiki na klabu ya Japan ya Urawa Reds.Kiasi cha mashabiki 300 wa Bayern Munich walifika uwanja wa ndege kuwakaribisha walipowasili.

Leo Munich inacheza na Urawa Reds –mojawapo ya timu za Ligi ya Japan.

Katika changamoto za Kombe la klabu bingwa barani Afrika,Enyimba ya Nigeria ilishindwa kuwika wazi mbele ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini na mwishoe, waliondoka uwanjani suluhu huko Aba,Nigeria, kwa bao 1:1.

Chidozie Johnson alisawazisha mnamo dakika ya 66 ya mchezo kuikoa Enyimba kutoaibishwa nyumbani.Ilikua mechi walioidhibiti barabara lakini walishindwa kutia mabao.Piarates ambao hawakuthubutu kukaribia eneo la adhabu la Enyimba, walitangulia ghafula kwa bao la Lucky Lekgwathi mnamo dakika ya 33 ya mchezo.

Enyimba ilitwaa ubingwa wa kombe hili 2003 na 2004 .Al Ahly ya Misri walizima ndoto ya Enyimba kutwaa taji hili kwa mara ya 3 mfululizo.

Al Ahly-mabingwa walikua pia uwanjani na wao waliikandika JS Kabylie ya Algeria mjini Cairo mabao 2:0.Asante kotoko ya Ghana, ilitamba nyumbani huko Obuasi ilipoizaba CS Sfaxien ya Tunisia mabao 4:2.

Katika mapambano ya kundi B, ASEC Mimosas ya Corte d’Iviore ilitandika Hearts of Oak ya Ghana Na kwemye changamoto za timu chipukizi barani Afrika, Mauritius ilitoka suluhu 0:0 na Reunion,lakini Reunion inasonga mbele kwa ushindi jumla wa mabao 4:1.

Mjini Asmara: Eritrea iliitoa Libya kwa mabao 2:0 na kwa ushindi jumla wa mabao 3-2,Eritrea inajiunga na Reunion duru ijayo.

Mjini Lusaka,Zambia ilitamba kwa mabao 2-0 dhidi ya Msumbiji na inasonga mbele kwa ushindi wa mabao 4:1.

Mjini Blantyre,Malawi ilikomewa mabao 2:1 na Lesotho,lakini kwa mabao 4-2,Malawi imetoroka na tiketi ya duru ijayo na kuwaacha nyuma chipukizi wa Lesotho.

Huko Afrika Mashariki,Tanzania ikijiandaa kwa Kombe la Afrika la mataifa 2008 nchini Ghana chini ya kocha mpya kutoka Brazil ilikuwa uwanjani jana ikipimana nguvu na Ruanda.Tanzania ilitoa Ruanda kwa bao 1:0.

Bingwa mara kadhaa wa mbio za magari, Michael Schumacher wa Ujerumani,amekuza nafasi zake za kuweza kuibuka tena bingwa wa mashindano ya magari ya grand Prix.

Kwa ushindi wa jana katika German Grand prix huko Hockenheim,Schumacher amepunguza mwanya wake na bingwa Fernando Alonso anaeongoza kwa pointi 17 kwa 11 za schumacher.Schumacher talari bingwa mara 7 aaania taji lake la 8.

Riadha:

Bingwa wa dunia na Olympic wa masafa mafupi mita 100,muamerika Justin Gatlin anakabiliwa na marufuku ya maisha katika mashindano ya riadha endapo ukaguzi wake uliogundua ametumia madama ya testosterone utathibitishwa na wakuu wa riadha wa Marekani-hii ni kwa muujibu wa shirika la riadha ulimwenguni-IAAF.

Gatlin pia ndie bingwa wa rekodi ya dunia pamoja na Asafa Powell wa Jamaica.Gatlin alifichua jumamosi kuwa amekutikana ametumia madama ya kutunisha misuri kuongeza kasi.