Bayern Munich yajihakikishia ubingwa wa kandanda
1 Mei 2005Matangazo
Bayern Munich imejihakikishia ushindi kama timu bingwa ya Ujerumani baada ya kuikandika Kaiserslautern mabao 4-0.Nafasi hiyo imeimarishwa pia baada ya timu ya Schalke inayoshika nafasi ya pili,kwenda sare na Bayer Leverkusen kwa magoli 3 ilipocheza nyumbani.Bayern Munich sasa inaongoza kwa pointi 11 huku michezo 3 ikibakia kuchezwa katika Ligi ya Ujerumani yaani Bundesliga.