1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern Munich na Real Madrid kuumana

18 Aprili 2012

Macho ya mashabiki wa soka, leo yanakodolewa kwenye pambano la nusu fainali ya kombe la ligi ya mabingwa Ulaya - Champions League, ambapo Bayern Munich ya Ujerumani inamenyana na miamba ya Uhispania Real Madrid.

https://p.dw.com/p/14fKY
Bayern's Mario Gomez celebrates after scoring his side's opening goal during the German first division Bundesliga soccer match between FC Bayern Munich and TSG 1899 Hoffenheim in Munich, Germany, Saturday, March 10, 2012. (Foto:Matthias Schrader/AP/dapd) NO MOBILE USE UNTIL 2 HOURS AFTER THE MATCH, WEBSITE USERS ARE OBLIGED TO COMPLY WITH DFL-RESTRICTIONS, SEE INSTRUCTIONS FOR DETAILS
Vorschau Bayern München Real Madrid Ronaldo vs Mario GomezPicha: dpa/AP

Kocha wa Bayern Munich Jupp Heynckes ana matumaini timu yake leo iatafanikiwa kuibwaga Real Madrid na hasa kwa kuwa Bayern itakuwa ikicheza nyumbani kwenye uwanja wa Alianz Arena katika pambano hilo la nusu fainali ya kwanza kabla ya mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo mjini Madrid.

Ni katika uwanja huo huo, ambako fainali ya kombe hilo la champions leagues itachezwa Mei 19. Heynckes alilinyakua kombe hilo wakati alipokuawa kocaha wa Madrid katika msimu wa 1997-98, ambapo walimaliza nafasi ya nne katika ligi ya Uhispania.

Kwa kuwa safari hii inaelekea Bayern haina nafasi ya kuutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Ujerumani ambapo Borussia Dortmund inajiandaa kuunyakua mawaka wa pili mfululizo, Heyckes anatarajia mbinu zake zinaweza kufua dafu na kushinda kombe la vilabu bingwa vya Ulaya.

Mario Gomez ataongoza safu ya mashambulizi ya Bayern Munich
Mario Gomez ataongoza safu ya mashambulizi ya Bayern MunichPicha: AP

Bayern tayari wameiaga Bundesliga

Heynckes mwenye umri wa miaka 66 ana uzowefu na timu za Uhispania na amewahi kuawa mkufunzi awa Athletico Bilbao 1992-94 na 2000 hadi 2003 alikuwa kocha wa Tenerife kabla ya kuifundisha Real . Lakini wakati Bayern haikuwahi kushindwa na Real nyumbani, Heynckes naye hakupata kuifundisha timu iliyoishinda ile ya Uhiospanaia katika mashindano ya Ulaya. Jee hilo leo litaabadilika?

Kocha wa Real Madrid Mreno Jose Mourinho naye anatamba kwamba atainyowa Bayern Munich, akiwategemaea wachezaji wake nyota kama Cristiano Ronaldo, Angel di Maria na Karim Benzema, huku Bayern ikiweaka matumaini kwa nyota Arjen Robben, Frack Ribery na Bastian Schweinsteiger.

Bila shaka mashabiki wa soka wameingiwa na kiwewe wakisubiri firimbi ya mwisho kuamua. Mwenzake Iddi Ismail Sessenaga ana maoni yafuatayo kuhusu pambano la leo.

Baada ya kuukosa ubingwa wa ligi kuu ya Ujerumani -Bundesliga akama inavyowelekea mikonononi mwa Borussia Dortmund , sasa Bayern inajizatiti kuona sio tu inalinyakua kombe la vilabu bingawa-champions league lakini pia Kombe la Ujerumani DFB ambapo itakutana n katika fainali na Borussia Dortmund mwezi ujao mjini Berlin.

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman/afp

Mhariri: Saumu Mwasimba