1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern kuumana na Atletico

2 Mei 2016

Mabingwa mara tano wa Champions League, Bayern Munich wanalenga kuepuka kubanduliwa nje na mpinzani wa kutoka Uhispania katika hatua ya nusu fainali kwa msimu wa tatu mfululizo

https://p.dw.com/p/1Igfp
Deutschland FC Bayern München Abschlusstraining in München
Picha: picture-alliance/dpa/A. Gebert

Bayern waliondolewa katika nusu fainali ya Champions League na miamba wa Uhispania Real Madrid 2014 na Barcelona 2015.

Bayern italenga kutumia faida ya mashabiki wa nyumbani uwanjani Allianz Arena kesho Jumanne dhidi ya Atletico Madrid ambao wanakuja Ujerumani na faida ya bao moja kwa sifuri. Guardiola aliwapumzisha Xabi Alonso, Javi Martinez, Philipp Lahm, David Alaba, Arturo Vidal, Thiago Alcantara, Douglas Costa na Robert Lewandowski katika mtannage wa mwishoni mwa wiki.

Siku ya Jumatano, Real Madrid itashuka dimbani dhidi ya Manchester City uwanjani Santiago Bernabeu. Swali kubwa ni je, Madrid ambao ni mabingwa mara kumi wa kombe hilo ni: je, Cristiano Ronaldo na Karim Benzema watakuwa katika hali nzuri kucheza? Ronaldo amefanya mazoezi kamili leo wakati Benzema anatiliwa shaka kama ataweza kuwa sawa.

Lakini Gareth Bale ametumia nafasi yao kwa kutamba. City wanakwenda Madrid wakiwa na faida ya uwezo wa kufunga bao la ugenini baada ya mkondo wa kwanza kukamilika kwa sare ya sifuri kwa sifuri.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu