Bayern kutwaa taji la Mabingwa walihitaji nguvu na akili.
24 Agosti 2020Ushindi wa bao 1-0 siku ya Jumapili dhidi ya Paris St Germain haukuwa tu kushiklia mataji sita ya Ulaya kwa Bayern, lakini pia iliwaonyesha wao kuwa timu ya kwanza kushinda mechi zote za ligi ya mabingwa katika msimu.
Katika mchezo huo wa fainali ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya, Bayern Munich iliweza kutwaa taji hilo baada ya kuitandika PSG bao 1-0 likiwekwa wavuni kwa njia ya kichwa na winga wa kushoto mrithi wa Ribery, Kingsley Coman.
Bado ilipaswa kuonekana kuwa ulikuwa msimu wa mpito kwa Bayern kufuatia kuondoka kwa mawinga wakongwe Arjen Robben na Franck Ribery na mabeki Mats Hummels na Rafinha mnamo mwaka 2019.
Safu ya ulinzi ambayo haikuwa madhubuti na utegemezi mkubwa wa mchezaji Robert Lewandowski katika safu ya ushambuliaji uliwafanya Bayern kutabirika kirahisi na hatimaye kutandikwa mabao 5-1 na timu ya Eintracht Frankfurt kulithibitisha kuwa pigo la mwisho la kuondolewa kwa kocha Nico Kovac na nafasi yake kuchukuliwa na kocha Hansi Flick mnamo mwezi Novemba.
“Tuliendelea kusonga katika msimu huu, tulikuwepo kila mmoja, tayari kusahihisha makosa ya kila mmoja,” alisema kiungo mshambuliaji Thomas Mueller, aliyekuwa akiwekwa benchi lakini amekuwa wa kuvutia chini ya kocha Flick. “Tuna ubora wa kushangaza lakini haifanyi kazi kama hauko tayari kuteseka. Nguvu zetu kiakili ni kubwa na kali.”
Miezi tisa tu baada ya kuchukua mikoba ya kuinoa Bayern Munich, Flick amekuwa tu kocha wa pili wa Ujerumani kushinda mataji matatu akifanya hivyo katika msimu wake wa kwanza kama kocha mkuu wa klabu hiyo ya Bundesliga.
“Wako njiani kwenda kuwa klabu kubwa zaidi duniani,” ameongeza Tuchel. “Wachezaji hawa wana sifa hizi za kushangaza na tayari wameimarisha timu yao.”
Soma Zaidi: Bayern Munich yatawazwa mabingwa Champions League