1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bata. Ndege yenye abiria 45 yapotea katika anga la Equatorial Guinea.

17 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEtu

Ndege moja ikiwa na abiria 45 imepotea nchini Equatorial Guinea katika Afrika ya kati. Ndege hiyo aina ya Antonov ilikuwa ikisafiri kutoka mji mkuu Malabo kwenda katika mji wa Bata ulioko bara. Ndege hiyo ilipotea katika rada muda mfupi baada ya kuruka.

Helikopta za kijeshi zinafanya msako kuitafuta ndege hiyo.