Baskeli yafikisha miaka 200: Karne mbili ya waendesha baskeli
Baskeli ilianza wakati mvumbuzi wake Karl Drais alipojaribu kutengeneza gari za mwanzo kwa mara ya kwanza miaka 200 iliyopita. Chombo hicho cha matairi mawili kimechukua sura nyingi tangu mwaka 1817.
Baiskeli ya kwanza yenye uwiano
Karl Drais alikuwa askari wa msituni, akiwa na elimu ya Fizikia na Hesabu. Baadhi ya vumbuzi zake ziliboreshwa na kukarabatiwa kwa kutumia mashine ikiwa ni pamoja na kigari alichobuni kisichotumia farasi ambacho baadae kilikuwa gari dogo lililotembea relini "railway handcar." Uvumbuzi wake mkubwa ulikuwa ni wa baisikeli ambao awali ukitokea magari yaliyosukumwa na binadamu ama "dandy horse".
Kutoka "dandy horse" hadi vélocipède
Mfaransa Pierre Michaux aliongeza pedali ama vikanyagio kwenye "dandy horse" mwaka 1861 kufanya kile kilichojulikana kama "Michauline". Pierre Lallement aliboresha zaidi ubunifu wake na kupatia hakimiliki "Lallement vélocipède." Hata hivyo haikuwa ya starehe. Gia ya mbele ilikuwa ngumu na kiti kilikuwa juu na kulikuwa na hatari ya mtu kuanguka.
Kuwa ya juu zaidi
Mwaka 1870, Mwingereza James Starley alifanikiwa kufika hatua nyingine ya kuboresha baisikeli. Ilioenakana kuwa na kasi kutokana na tairi kubwa la mbele. Hata hivyo haikuwa imara na waendeshaji walihitaji msaada kuipanda. Kuanguka kungesababisha majeraha makubwa. Baadae, Starley aliboresha mnyororo wa kwanza.
Ziara ya kwanza ya Ufaransa
Mwaka 1890, baiskeli zilizotajwa kuwa salama zikiendeshwa na waendeshaji wengi zikiwa na viti vya chini. Kukiwa na modeli hii ya kisasa, tukio maarufu zaidi la waendesha basikeli lilikuwa ni hili la ziara ya Ufaransa lililozinduliwa Julai 1,1903 mjini Paris. Mfaransa, Maurice Garin (aliyeko pichani katikati) alishinda mbio za Kilomita 2,428.
Mbio kwenye vifusi vya baada ya vita
Lilipokuja suala la kutengeneza maisha kwenye masalia ya vita vya pili vya dunia kuwa yanayowezekana, watu walijifunza kuwa wavumbuzi kwupitia kile kilichokuwepo. hakukua na shughuli yoyote ya starehe baada ya vita nchini Ujerumani. Mjini Berlin mnamo mwaka 1953, vijana wadogo walitengeneza njia ya kuendeshea baskeli kwenye kifusi.
Baskeli kama stuli
Mchezo wa soka unaendelea kuchezwa upande mwingine wa ukuta huu huko Vienna. watazamaji walitumia baskeli zao kama stuli kuangalia mchezo huo. Tukio hili la kihistoria limekuwa likirudiwa mara nyingi. Katika tamasha la AC/DC, Cologne la mwaka 2015, bendi ilitoa burudani katika uwanja uliozungushiwa uzio, wakati mamia ya watazamaji wasio na tiketi wakisimama kwenye basikeli zao wakifurahia tamasha.
Baskeli aina ya "Tandem plus three"
Picha hii iliyochukuliwa mwaka 1895 inaonyesha watoto watano wa Adam Opel. Walikuwa ni wakimbiaji wa mbio za baskeli waliofanikiwa sana na kufanya baskeli ya Opel kuwa na umaarufu. Opel akaanza kutengeneza baskeli mwaka 1886 na kuwa mzalishaji mkubwa duniani ilipofika miaka ya 1920. Kampuni yake kwa sasa inafahamika zaidi kwa magari yake, ambayo ilianza kuyatengeneza mwaka 1899.
Baskeli nzito zaidi duniani
Frank Dose ameweka rekodi ya kuunganisha baskeli na kuwa nzito zaidi duniani. Ilikuwa na uzito wa Kilo 1,080, na aliiendesha mita 100 kwa nguvu zake mwenyewe. Alipata wazo baada ya kunywa bia chache kwenye tamasha moja lililohusiana na vifaa vizito vya chuma. Dose alihitaji tu vyuma chakavu na matairi ya lori. Na muhimu zaidi ni vitairi vidogo vya nyuma- Sio baskeli ambayo ungetaka kuitamani.
Unaweza kuendesha na hii pia
Mbunifu Dieter "Didi" Senft anatambulikana kwa ubinifu wa baskeli yake ambayo si kawaida. Lakini pia amefanikiwa kutengeneza rekodi mbalimbali mpya kwa ubunifu wake. Baskeli hii ilitengenezwa na reki za bustani 111, ina urefu wa mita 4 na mita mbili kwenda juu. Hii pia unaweza kuendesha: Ina kiti cha ambacho unaweza kukaa na kuendesha baskeli kwa miguu.
Kuendesha kwa pande tofauti
Mtaalamu wa baskeli Ulrich Teige pia amejikita katika ubunifu wa ajabu ajabu. Katika makumbusho yake ya Pedalwelt huonyesha baskeli za ajabu kama ya kuendesha kwa pande tofauti kama hiyo: baskeli ambayo huenda kule ambako mtu husukumia pedali mbele, na mwenzake akiendeshea kwa kwenda nyuma.
Imara na rafiki wa mazingira
Baskeli za miti ya mianzi sio tu ni imara, bali pia zinaweza kutumika kwa safari ndefu. Karina na Tim Poser (pichani) walisafiri na baskeli kama hiyo kutoka Hamburg hadi mji wa Chengdu ulioko China. Baskeli zilizotengenezwa na wafanyabiashara wa Ghana na Ujerumani, zilitembea urefu wa Kilomita 12,000 bila ya tatizo lolote kubwa.
Mvuto wake kwa watu ndio kitu cha msingi
Hadi sasa, hakuna kikomo cha ubunifu unaowezekana. Baskeli zinazoweza kuendeshwa na mtu akiwa amelala zinawezesha mwendeshaji kukaa akiwa amejiegemeza mgongo. Kuna baskeli ndefu pia na nene zenye matairi manene. Aina hizi baskeli ni za starehe na huvutia. Mfumo wake wa mzunguko na mitindo ya za ajabu huzifanya kuwa na baskeli zinazotangazwa kuwa maarufu sana.
Kunywa na endesha: Baskeli ya "Bia"
Kaunta ya bar iliyotengenezwa kwa miti, chupa za bia na muziki. baskeli ya aina hii inaweza kuendeshwa na hadi watu 10. Bar hii inayotembea imekuwa tishio kwa usalama wa barabarani katika miji ya Ujerumani. Waendeshaji mara nyingi walikuwa walevi na kushindwa kuendesha kwa usalama: Ndio maana hivi sasa wamepigwa marufuku katika miji mingi.
Baskeli ya miguu mitano.
Huu ni mfano mwingine wa ubunifu. Katika mashindano ya Olimpiki ya majira ya joto ya mwaka 2008 mjini Beijing, Mchina huyu aliongezea matairi ya rangi tofauti kwenye baskeli yake yaliyoonyesha alama ya Olimpiki.
Waendesha baskeli Milioni tisa
Beijing ndio inashikilia rekodi ya kuwa mji mkuu wenye idadi kubwa ya baskeli. Magari pia yamejaa katika mji huo mkuu wa China. Kama mmtu angeweza kutakiwa kubuni idadi ya baskeli ambayo bado inaendeshwa katika mji huo, wengi wangependezwa na tukio la Katie Melua la mwaka 2005 la "baskeli Milioni tisa".
Njia ya kimataifa ya Usafirishaji
Viwango kadhaa vinajaribu kuonyesha miji rafiki kwa waendesha baskeli duniani.Mji wa Addis Ababa, Ethiopia, ambako watu hupita barabara za mashimo, mifugo na madereva wasiofuata sheria, inaweza kushika nafasi ya mwisho. Wamiliki wa mifugo wasio waoga, hubeba mifugo wakiwa wanaendesha baskeli. Mji mkuu wa Denmark, Copenhagen umechaguliwa kama mji ambao ni rafiki azidi kwa waendesha baskeli
Aina mpya ya kutembea: Baskeli ya kukunja
Haikuwa rahisi sana kwa baskeli za kukunja kwa miongo kadhaa iliyopita. Zilikuwa nzito na ngumu kuendesha. Aina mpya ni rahisi kukunja na kuwa kitu kidogo na rahisi kuibeba na inaweza kufikia spidi ya kawaida inapokuwa barabarani. Ni baskeli zinazotambulika kwenye magari ya usafiri, kwa kuwa zinaweza kubebwa kwa urahisi kwenye mabasi ama treni bila ya gharama za ziada.
Wazimu wa Waingereza
Baskeli za kukunja maarufu, Bromptom huko Uingereza zimefikia kiwango cha kama madhehebu si tu Uingereza, bali pia Japan na Marekani. Ni baskeli za kukunja. Shukrani kwa gia zake za kisasa, na ni baskeli inayokwenda kasi kuliko inavyoonekana. Kuna mbio za baskeli hizo kila mwaka London na New York. Katika matukio hayo, waendesha baskeli si tu hutakiwa kwenda kasi, lakini pia huwa na mavazi nadhifu
Zimetengenezwa kuendana na mazingira
Kuna aina za tofauti za baskeli zinazotumia mashine ya kuendeshwa. Baadhi zina nguvu sana, na hazihitaji kusukumwa kwa miguu kwa kuwa kifaa kilichowekwa huongeza nguvu kwenye pedali kumsaidia mwendeshaji. Ingawa zina sifa kwamba ni za wanaojiweza. Kuna aina tofauti hivi sasa kwa ajili ya waendesha baskeli kama maeneo ya milimani. Baskeli nzuri huuzwa hadi Euro 2,500 nchini Ujerumani
Ndoa kwenye baskeli
Mkataba wa upendo kwenye baskeli: wakati wengi wakikodisha magari ya kifahari kama limousine kuwabeba kwenye harusi ama magari yanayovutwa na farasi, hawa walichukua baskeli na kuendesha kwenda kwenye "Honeymoon". Baskeli ya kubeba wanaharusi zinapata umaarufu, hata miongoni mwa watu maarufu. dada yake Beyonce, Solange Knowles na mchumba wake walitumia baskeli walipokuwa wakienda kufunga ndoa.