1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Barcelona yatawala timu bora ya mwaka Ulaya

8 Januari 2016

Wachezaji wa klabu bingwa ya Ulaya na ulimwengu Barcelona wamemaliza karibu nusu ya kikosi cha Timu Bora ya Mwaka barani Ulaya huku Cristiano Ronaldo akijumuishwa kwenye kikosi hicho kwa mara ya kumi ikiwa ni rekodi mpya

https://p.dw.com/p/1HaNQ
FIFA Club World Cup Finale - FC Barcelona vs. River Plate
Picha: picture-alliance/dpa/K. Ota

Wachezaji nane kutoka ligi ya Uhispania La Liga walijumuishwa kwenye kikosi kamili cha wachezaji 11, kilichopigiwa kura na watumiaji milioni 7.2 wa tovuti ya UEFA.com kutoka orodha kali ya wachezaji 40.

Lionel Messi, Dani Alves, Gerard Pique, Andres Iniesta na Neymar ni wachezaji wa Barca waliojumuishwa, wakati Real Madrid ikiwakilishwa na Ronaldo, Sergio Ramos na James Rodriguez.

Mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich waliwakilishwa na mlinda mlango Manuel Neuer ana David Alaba huku mchezaji pekee aliyechaguliwa kutoka ligi kuu ya Italia, Serie A akiwa ni Paul Pogba wa Juventus. Pogba ni mmoja wa wachezaji watatu waliochaguliwa kwa mara ya kwanza pamoja na Neymar na Rodriguez.

Premier League ya England iliambulia patupu, licha ya kuwa na misuli ya kifedha na majina makubwa kama vile Sergio Aguero na Yaya Toure wa Manchestet City, Alexis Sanchez wa Arsenal na Eden Hazard na Diego Costa wa Chelsea

Timu kamili.

Mlinda mlango: Manuel Neuer (Bayern Munich and Germany).

Mabeki: David Alaba (Bayern Munich and Austria), Sergio Ramos (Real Madrid and Spain), Dani Alves (Barcelona and Brazil), Gerard Pique (Barcelona and Spain).

Viungo: Andres Iniesta (Barcelona and Spain), Paul Pogba (Juventus and France), James Rodriguez (Real Madrid and Colombia).

Washambuliaji: Lionel Messi (Barcelona and Argentina), Neymar (Barcelona and Brazil) and Cristiano Ronaldo (Real Madrid and Portugal).

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Iddi Sessanga