1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Barcelona yaiduwaza Madrid kwa kuitwanga 4-0

21 Machi 2022

Mfululizo wa vichapo kwa Barcelona dhidi ya Real Madrid hatimaye ulifikia kikomo jana wakati klabu hiyo ya Catalunya ilipata ushindi mnono wa 4 – 0 dimbani Santiago Bernabeu

https://p.dw.com/p/48nIT
Fußball Real Madrid - FC Barcelona 0:4
Picha: NurPhoto/IMAGO

Barca iliendeleza kasi yake ya hivi karibuni chini ya Xavi Hernandez katika mechi ya mwisho ya El Classico msimu huu. Barca walikuwa wamepoteza mechi tano mnfululizo dhidi ya hasimu wake huyo wa na sasa huenda wana nafasi ndogo ya kushinda ubingwa baada ya mwanzo mgumu wa msimu wao bila ya Lionel Messi. Alipoulizwa kama Barca ya zamani imerudi, Xvi alisema "Labda ndiyo. Ni juu yenu. Lakini tumejiambia kuwa hii ndio njia ya kufuata, na huu ndio muundo wa mchezo ambao tunataka kufuata. Hivi ndivyo Barca inapaswa kucheza na kushindana, na kwa wachezaji tulio nao, tuna wachezaji ambao ni wazuri sana kwa mtizamo wa kiufundi."

Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti amesema inasikitisha namna walipoteza mchezohuo lakini watafanya marekebisho wakati huu ambao ligi imeingia mapumziko mafupi kwa ajili ya mechi za kimataifa. "Sasa tuna faida ya pengo la pointi tisa kileleni, na tuko katika robo fainali ya Champions League. Naelewa kichapo hicho, Nakifahamu zaidi. Naomba radhi, Nimekasirika sana na nina huzuni, lakini napaswa kuwa mtulivu na kutafuta usawa wa hali hii, na naupata usawa huo katika faida ya pengo la pointi tisa tulilo nalo.

Barcelona ina pointi 54 sawa na nambari nne Atletico Madrid na pointi tatu nyuma ya nambari mbili Sevilla, ambayo ilikabwa kwa sare tasa na Real Sociedad.

afp