BARCELONA: Washukiwa ugaidi wamekamatwa Hispania
27 Juni 2007Matangazo
Wanaume 3 wanaotuhumiwa kuajiri watu watakaoweza kutumiwa kama magaidi kwa niaba ya mtandao wa al-Qaeda,wamekamatwa nchini Hispania.Polisi imesema, wanaume hao watatu walikamatwa mjini Barcelona na wanahusika na kundi linaloitwa,“Shirikisho la al-Qaeda katika eneo la Kiislamu la Maghreb“.Hivi karibuni,maafisa wa Ulaya wanaopambana na ugaidi, walionya kwamba chama kilichokuwa na makao yake nchini Algeria,kinajaribu kueneza harakati zake barani Ulaya.