1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Barcelona mabingwa wa Kombe la Mfalme

23 Mei 2016

Licha ya Barcelona kubanduliwa nje ya Champions League katika hatua ya robo fainali, kocha Luis Enrique amesema ushindi wao dhidi ya Sevilla katika fainali ya Kombe la Mfalme umeukamilisha msimu wenye mafanikio

https://p.dw.com/p/1It8m
FC Barcelona gegen FC Granada Liga BBVA 2015 2016 38. Spieltag spanische Meisterschaft
Picha: picture-alliance/AP Photo/D. Tejedor

Barca iliwapiku Sevilla mabao mawili kwa sifuri baada ya muda wa ziada ushindi ambao kocha Enrique amesema walistahili "Tulistahili kushinda fainali. Ni zawadi ya haki kwa timu ambayo imetengenezwa kushambulia lakini ilistahili kujikinga na kuumpa mpinzani mpira. Walijua namna ya kuziba mianya na kushambulia. Wameweza kuonyesha ushindani mkali na kucheza kandanda kitu ambacho ni muhimu kwa kila timu. Hili linatufanya kujivunia kwa hivyo tuna furaha kubwa maana msimu wa joto unaanza.

Kwa kulitetea kombe la Mfalme, Barca sasa wameshinda taji la saba katika mashindano tisa chini ya Luis Enrique. Kocha wa Sevilla Unay Emery aliwapongeza vijana wake akisema ushindi wao wa kombe la Europa League Jumatano wiki iliyopita dhidi ya Liverpool mjini Basle, uliwapa muda mdogo wa kujiandaa.

Kando na taji la La Liga msimu uliopita, Kombe la Mfalme na Champions League, walishinda pia UEFA Super Cup na Kombe la Klabu Bingwa duniani chini ya Enrique.

Mwandishi: Bruce Amani/DPA/AFP
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman