Barca yaendelea kutawala kandanda Uhispania
16 Februari 2016Lakini gumzo katika mchezo huo ni mkwaju wa penalti alioufunga Suarez baada ya kukatiwa pande laini na lionel Messi. Upigaji huo wa penalti kwa kumpa basi mfungaji badala ya mpambano kati ya mlinda mlango na mpigaji umekuwa gumzo kubwa na mjadala unaendelea kwamba je wachezaji wa Barca walionesha dharau kwa wenzao wa Celta Vigo ama vipi.
Mashabiki nchini Uhispania na duniani kwa jumla wamegawanyika kuhusu hilo , wengine wakisema ni sahihi na wengine wakisema ni dharau. Sheria haisemi chochote kuhusu timu inayoshindana na mwenzake kufanya dharau uwanjani iwapo timu nyingine imefungwa. Lakini ni jambo la ubinadamu kumheshimu mpinzani wako hata kama amemgaragaza kwa kumpaka tope , lakini ni muhimu kumheshimu.
Ufungaji huo hauna ubishi, ni jambo la kawaida kufunga kwa njia hiyo, lakini suali linaulizwa je ni vizuri kumdhalilisha mpizani wako kiasi hicho? Kama ni kumdhalilisha ama la pia ni suali linalojadilika.
Barca ina pointi 57 na inaingia tena uwanjani siku ya Jumatano kupambana na Sporting Gijon katika mchezo ulioahirishwa Desemba mwaka jana kutokana na klabu hiyo kushiriki michuano ya kombe la dunia la vilabu . Na iwapo Barca itashinda mpambano huo itakuwa na sita zaidi ya timu inayoifuata Atletico Madrid.
Mwandishi : Sekione Kitojo / rtre / dpae /zr /
Mhariri: Mohammed Abdul Rahman