Baraza la Wawakilishi Marekani lashindwa kuchagua spika
4 Januari 2023Katika duru ya kwanza, wajumbe 19 waliasi kutoka chama chake na katika duru mbili zilizofuatia, McCarthy alishindwa kupata kura za kutosha kutoka kwa Warepublican wenzake.
McCarthy amewaambia waandishi wa habari kuwa rais wa zamani, Donald Trump, alimpigia simu na kusisitiza kumuunga mkono, lakini kilichoshuhudiwa bungeni sicho alichokitarajia.
"Kuna mambo mengi tulitaka kufanya. Tulitaka kuweka idadi ya kesi za uchunguzi tulizonazo. Tulitaka kuona vikao mbalimbali vya kamati tulizonazo. Hakuna kati ya hayo kilichotendeka. Lakini kama tutaweza kutatua tofauti zetu, na mara hii tufaulu, tutakuwa na nguvu zaidi na kukamilisha mambo tunayotaka kuyafanya," amesema McCathy
Mwanasiasa huyo kutoka California alihitaji kura 218 kati ya 434. Hii ni mara ya kwanza katika karne moja, kwa Warepublican kushindwa kumchagua spika hata baada ya majaribio matatu.