SiasaAfghanistan
Baraza la Usalama laomba ushauri wa kukabiliana na Taliban
17 Machi 2023Matangazo
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa aidha limeomba kushauriwa namna linavyoweza kupambana na changamoto ikiwemo ukandamizaji wake wa haki za wanawake na wasichana. Baraza hilo lenye nchi 15 wanachama lilipitisha kwa kauli moja azimio linalomhitaji Guterres kuwasilisha ripoti katikati ya mwezi Novemba, ikiwa na mapendekezo ya mbinu za kufanya kazi na utawala huo katika nyanja muhimu kama siasa, kibinaadamu na maendeleo ndani na nje ya Umoja wa Mataifa. Utawala wa Taliban uliochukua madaraka Agosti mwaka 2021 wakati wanajeshi walioongozwa na Marekani kuondoka nchini humo baada ya miaka 20 ya vita, unasema unaheshimu haki za wanawake chini ya tafsiri yake ya sheria za kiislamu.