Baraza la Usalama lahofia "kutanuka ghasia" Kongo Mashariki
13 Februari 2024Matangazo
Wajumbe wa baraza hilo waliokutana jana Jumatatu, wamerejea matamshi yao ya kuyalaumu makundi ya wapiganaji yanayoendesha operesheni zao nchini humo kuwa chanzo cha kudodora hali ya usalama upande wa mashariki.
Wamesisitiza msimamo wao wa kuiunga mkono Kongo katika kulinda uhuru wake na kuheshimiwa hadhi ya mipaka ya taifa hilo.
Serikali ya Kongo, Umoja wa Mataifa na nchi za magharibi zinaituhumu Rwanda kuwaunga mkono waasi wa M23 kwa dhamira ya kudhibiti utajiri wa madini mashariki mwa Kongo.
Kundi hilo la waasi limeyakamata maeneo makubwa mashariki mwa Kongo tangu lilipozukla tena mwaka 2021 na sasa linatishia kuuchukua kwa mara nyingine mji wa kimkakati wa Goma.