Baraza la Usalama la UN lakutana kuzungumzia uchaguzi DRC
4 Januari 2019Matangazo
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakuwa na kikao cha siri leo kuzungumzia uchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Kikao hicho kilichoitishwa na Ufaransa kitaanza leo usiku wakati jumuiya ya kimataifa ikisubiri matokeo ya uchaguzi ulioitishwa Jumapili iliyopita.
Marekani imetoa wito matokeo sahihi ya uchaguzi yatangazwe na kuwataka viongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo waondowe vizuwizi vilivyowekwa dhidi ya mitandao.
Madola ya magharibi pamoja pia na nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wameelezea matumaini yao kuiona nchi hiyo kubwa kabisa ya kusini mwa jangwa la Sahara ikishuhudia kipindi cha amani cha mpito, kwa mara ya kwanza tangu uhuru mwaka 1960.