Baraza la usalama UN lahimiza msaada wa usalama kwa Haiti
15 Julai 2023Matangazo
Katika mkutano wake, baraza hilo la Umoja wa Mataifa, lilipitisha azimio la kurefusha kwa mwaka mmoja jukumu la ujumbe wa kisiasa wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti. Azimio hilo pia liliunga mkono wito wa msaada wa usalama kwa polisi wa nchi hiyo.
Soma zaidi: Guterres atoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuyapa kipaombele mahangaiko ya watu wa Haiti
Baraza hilo lenye wanachama 15, linayahimiza mataifa wanachama pamoja na mataifa katika eneo hilo kutoa msaada wa kiusalama kwa jeshi la polisi la Haiti ikiwa ni pamoja na kupeleka kikosi maalumu. Pia limemtaka Guterres kuwasilisha ripoti kwa baraza hilo ndani ya siku 30, kwa kushauriana na Haiti, kuelezea kikamilifu aina ya misaada ya Umoja wa Mataifa.